Trevor alihisi mtu akimuangalia na akaangalia upande wa mlango. Ilikuwa ngumu kuuficha mshangao wake alipomuona Quinn Wilder na Warren Santos. Ikiwa hakuwa anashuku aliyoshuku, Trevor angeamini kuwa wawili hao walihusika kwenye mauaji na walikuwa wakipanga hatua yao yakufuata. Lakini wazo hilo lilikuwa la wale wapumbavu waliokuwa kwenye kikosi cha polisi.
“Mwenye Mwanga wa Usiku anafanya nini hapa?” Trevor aliuliza akimgeukia Kat.
“Sote tunajaribu kulitatua tatizo la wafyonza damu,” Kat alisema wakati akimkazia Quinn macho. Oh, alionekana kutingishika kidogo. Ilikujaribu hoja hiyo, alisongea karibu na Trevor kana kwamba alikuwa akimnong’onezea maneno matamu masikioni, “Je, una silaha yoyote tunaweza kutumia kuusawazisha uwanja?” alimkonyezea jicho akijua kuwa ameisha mpata mwenzake kwa usiku wa leo.
Trevor aliliwaza hilo kwa muda, akipiga hesabu kichwani mwake kuhusu kile alichokuwa nacho kwenye gari lake.
“Ndio, nina vifaa kadha kwenye gari,” Trevor alisema. “Huenda ikabidi turudi kwangu nyumbani kuongezea vyengine nilivyo weka kwenye kasha yangu ya bunduki.”
‘Vizuri,’ Kat alifikiria.
Wakati Warren na Quinn walipokuwa wakitembea kuipita baa, Warren kwa mara nyengine aliitwa na kile kifaa cha mawasiliano masikioni mwake. Quinn hakujali kule kuchelewa. Kulimpa muda wa kuchunguza kilichokuwa kikiendelea kati ya watu wawili walikuwa na furaha pale kwenye baa.
Kat alimuona Quinn akija na kwa haraka aliiteremsha baa ili Trevor asisikie na Quinn asiitoboe siri yake. Akiifikia chupa, aligeuka na kumpata Quinn amesimama kati yake na baa.
“Je, ninaweza kukusaidia?” Kat aliuliza kwa kejeli na kuinua unyusi. “Unajua kuwa hakuna wateja wanao ruhusiwa nyuma ya baa.”
Quinn alichukua hatua mbele ingawa tayari mahali pale palikuwa pamefinywa sana. Akiuweka mkono kando ya mkono wa Kat, alimbana mahali alipokuwa. Akiona macho yake yakiangalia juu ya mabega yake kumwelekea yule mtu aliyekuwa akiongea naye… Quinn alinguruma, “Usipoteze nira usiku wa leo Kat. Ninakuonya. Kwa sababu hauji nasi kuwinda haimaanishi kuwa mfyonza damu hawezi tu kuingia kwenye mlango wa baa hii.”
Kat alivuta pumzi akijua kuwa hiyo ndiyo ilikuwa mbinu ya kale zaidi kitabuni. Kumfanya mtu afikirie kuwa walikuwa muhimu kwa kuwapa kazi salama ya kando. “Nitakuwa sawa,” alimwambia akipita chini ya mkono wake na kuelekea upande alikokuwa Trevor. “Na niki hitaji chochote, tayari kunaye mtu aliye tayari kunipa.” Hilo la mwisho lilitamkwa na sauti iliyokuwa ya kutongoza. Ulikuwa uongo, lakini Quinn alikuwa amemkasirisha.
Alitabasamu akijua kwa ndani kuwa Quinn alifikiria kuwa alimaanisha kingono na Trevor alifikiria kuwa alimaanisha ule uwindaji wa wafyonza damu usiku wa leo. Warren alichagua muda huo kumalizia na kumuashiria Quinn kuwa alikuwa tayari kutoka.
Midomo ya Quinn ilibana wakati alipotembea nyuma ya Kat na kuinama chini, karibu kuigusa midomo yake kwenye masikio yake, “Kuwa na usiku salama.” Alitazama wakati msisimko ukienea kwenye shingo na bega la Kat kwa kutosheka.
Kat aliushika upinde wa baa wakati magoti yake yalipokosa nguvu. Akijiinua aliruka wakati sauti ya Michael ilikuja kutoka nyuma.
“Mpendwa, kuwa muangalifu jinsi unavyo vuta mkia wa pake yule,” Michael alimkumbusha kisha akatikisa kichwa kuelekea alikokuwa Trevor kabla ya kuenda kukutana na Kane juu ya paa.
Trevor alikunja uso kwa ule mshangao uliokuwa kwenye uso wa Kat. “Kwani yule hakuwa mfyonza damu?”
“La, yule alikuwa muungwana na anatusaidia kuwatafuta wanyama halisi” Kat alisema kwa ujasiri wakati akiongeza kimya kimya, na ndiye pekee ambaye hakuwa na pingamizi kuhusu mimi kuenda nje usiku wa leo. “Hata hivyo, inaonekana kana kwamba tunachelewa. Uko tayari kuondoka?”
*****
Kane alikuwa akitembea tembea kwenye paa, akivuta sigara na mara kwa mara akiirusha mikono yake hewani. Alikuwa akianza kuchoshwa na kumsubiri Michael afike.
“Chui na simba,” alinguruma. “Ni wabaya kuliko paka wa nyumbani. Kila mmoja lazima ammiliki mwengine. Afadhali ni ungane na mbwa mwitu badala ya kukabiliana na haya.”
Michael alitokea nyuma ya Kane pale kwenye ukingo wa paa, na kumpata akiwa kwenye hali yake ya kuropoka kwa hasira. Alikunja uso wakati Kane alikimya ghafla na kuangalia upande wake.
“Kane, je, tutaongea kuhusu kinacho kusumbua au la?” Michael aliuliza akimsongelea Kane.
“Au la,” Kane alijibu.
“Sawa,” Michael alisubiri akijua kuwa kane alichukia kunyamaziwa zaidi ya kubishana. Alipenda kila wakati akiwa sawa.
Kane alitembea kuelekea ukingoni mwa jengo, akiweka nafasi kati yao. Alikuwa amesahau jinsi Michael angeweza kumnyemelea… haikuwa imefanyika kwa muda mrefu. “Raven alionekana kukata tamaa kuwa kundi lake halikuwapo kwenye bohari… baadhi ya wenda wazimu wake walikuwa hawapo. Nina kisia kuwa wale wafyonza damu walio kosa karamu yetu ya kifo walihitaji mahali pa kushindia, kwa hiyo ninaenda kupaangalia.”
Michael hakusema neno lolote wakati Kane kwa mara nyengine alianguka chini upande wa paa na kutua chini kwenye barabara. Aliposongea ukingoni ili kujiangusha kama alivyofanya Kane, kitu kwenye paa nyengine upande wa pili wa barabara ulishika macho yake.
Akiyageuza macho yake kukielekea, Michael aliona kivuli tu wakati kikipotea. Kitu kuhusu kivuli hicho kilionekana kama alichokijua lakini hakuweza kujua ni nini hasa.
Kwani Kane alikuwa na mtu aliyekuwa akimnyemelea au yeye ndiye aliyelengwa? Akijaribu kuizuia hisia ile kwa sasa, aliangalia chini na kutabasamu alipoanguka. Ingawa alikuwa hawezi kumuona tena Kane, na aliijua njia ya kuelekea kwenye bohari, badala ya kuifuata njia aliufuata mvuto wa damu yake mwenyewe kwenye mishipa ya Kane. Wakai alipofika kwenye bohari, aliisikia milio ya wafyonza damu walio vamiwa na Kane wakiwa wamezubaa.
Alisita pale mlangoni akitumia uwezo wake wa kuona uliyokuwa wa juu ilikuona kwenye chumba kikubwa kilichokuwa na giza. Kane tayari alikuwa na wafyonza damu wawili juu yake na wengine zaidi walidhani kuwa mbinu ya kuvuta kama kundi moja kuwa wazo zuri. Akiingia ndani, aliufunga mlango nyuma yake na kuanza kusongea mbele wakati alipoisikia sauti ya Kane ikisema.
“Niwache nishughulikie hili. Hakikisha tu hakuna yeyoe atakayekupita hapo,” Kane alisema akivuta pumzi kwa nguvu akiivunja shingo ya mfyonza damu aliyekuwa akijaribu kuirarua koo yake. Alishtuka wakati meno yalipoingia kwenye bega lake, kumsababisha kumuachilia yule wa kwanza.
Nyusi zote mbili za Micheal zilipotea kwenye nywele zake lakini aliji alijibana kwenye mlango. “Sawa, ikiwa unahakika.” Aliikunja mikono yake kifuani mwake na kutegemea nyuma kwenye ile chuma.
“Nimesinywa,” alisema baada ya mud ana kuangalia upande wa wale wafyonza damu wasiyokuwa na nafsi ambao walikuwa hawajaingia kwenye vita. “Natumai mmoja wenu atanipa heshima ya kukimbia?”
Wakati Kana alipofaulu kumrarua yule mfyonza damu wa kwanza, mmoja aliyekuwa kando aligeuka na kukifanya kile ambacho Michael alikuwa amekipendekeza, lakini mikono ya Kane ilimfikia kwa kabuti yake ya ngozi aliyokuwa ameivaa. “Sidhani kuwa itakuwa hivyo,” alinguruma alipomvuta kule kwenye vita.
“Je, mama yako hakukufundisha kushiriki na wenzako?” Micheal alitabasamu alipomuona Kane akipigwa vibaya. Alihisi kuwa kwa sasa Kane alihitaji ule uchungu ilikuhisi kuwa yuko hai. Alikuwa hana shaka kuwa Kane ndiye atakaye kuwa mfyonza damu atakaye baki akiwa amesimama na huku kuwachilia hasira na fujo huenda hata kukamsaidia rafiki yake kufunguka tena… Tiba kamili.
“Mama yangu alikuwa mwizi,” Kane alijibu, akiruka juu na kuisukuma miguu yake yote miwili ndani ya kifua cha mfyonza damu aliyekuwa akikimbia kumuelekea. Mfyonza damu huyo aliruka na Kane alianguka kwenye mgongo wake. Akiirusha miguu yake juu, alisimama tena kwa miguu yake mara moja. “Hakuamini katika kushiriki.”
“Sote wawili tunajua kuwa mama yako hakuwa mwizi,” Michael alijibu.” Alikuwa mwangana aliyepata malezi mazuri.”
Kane alipigwa ngumi usoni na kurudi nyuma. Michael aliufata mwendo huo wakati Kane alipoolea kumpita na kuingia kwenye furushi la taka ambalo Kriss alimrusha hapo awali. Alishusha pumzi wakati alipoona kuwa Kane alikuwa akigeuka kuwa mchafuko wad amu. Kane aliingia kwenye vita tena, akiwararua wale wanaharamu akienda.
“Unahitaji msaada?” Michael aliuliza juu ya sauti za mifupa ikivunjika na miguu ikipigapiga kwenye vidimbwi ambayo ilikuwa ikiendelea kuwa mikubwa kila dakika. Alicheka wakati Kane alipoanza kunong’oza moja wapo ya fingo za Syn lakini alipigwa ngumi mdomoni kabla ya kuimaliza.
“Hapana,” Kane alinguruma akitema damu usoni wa yule aliyempiga ngumi kwa nguvu hadi akaona nyota. Akishika sehemu ya mbao kutoka kwenye kiti walicho kivunja wakati wa vita vyao, alikiingiza kwenye mdomo wa mfyonza damu kwa nguvu hadi kikatokea nyum ya shingo yake.
Michael alibadilisha sura lakini hakuingilia. Aliangalia kwa karibu, akihesabu wafyonza damu watatu waliokuwa chini na kubakia wanne. Kane alikuwa mpiganaji asiyekuwa na uoga, zaidi sasa kuliko kabla ya kuzikwa hai. Jambo lililomkumbusha Michael kuhusu swali moja ambalo alikuwa haja liuliza bado; Kane alilifunja vipi fingo la kufunga bila damu ya mwenzi wake war oho?
Chini ya dakika ishirini baadaye, Kane alianguka magotini. Akiangalia kupitia wingu lekundu machoni mwake kuelekea upande wa sauti ya mikono iliyokuwa ikipigwa ambayo ilikuwa ikisongea karibu. Aliifuta damu kutoka mdomoni mwake na kujaribu kujiinua kutoka sakafuni. Alicheka wakati hakuweza kujiinua kwa sababu sakafu ilikuwa ilikuwa inateleza kwa kuloa damu.
“Na mshindi anapata bandeji mia na usingizi mzuri usiku nyumbani mwa Michael.” Aliinama na kuizungusha mikono yake kwenye kiuno cha Kane kumsaidia kusimama. Waliteleza wote kable ya kusimama.
“Una nyumba?” Kane aliuliza akitumai kuwa akiendelea kuongea hatazimia kabla wafike huko. Aliju alikoishi Michael, lakini hakutaka kulikiri kwa sababu hilo lingemkumbusha tu Michael kumkasirikia kwa ku kaa mbali naye. Hakufurahishwa na jambo hilo mwenyewe lakini alihisi haja ya kujiweka mbali.
“Ndio, nime komaa sasa. Kando na hilo, majeneza ni mambo ya kale sana.” Alijikunja kwa ndani akitambuwa kuwa Kane huwenda alifikirie kuwa msaha ule ulikuwa huchekeshi. “Mahali ni pakubwa. Palikuwa aina ya jumba la hifadhi hadi walipojenga moja iliyoboreshwa huko Beverly Hills. Pengine ukihamia kwangu, mahali hapo patakuwa kama nyumba.”
“Ninataka mtoto wa mbwa,” Kane alisema ghafla akiweka umakini kwenye kuweka mguu mmoja mbele ya mwengine, hali ambayo hukufanya usianguke.
“Unamtaka nani?” Michael aliuliza.
“Ikiwa tutaishi pamoja, basi nitamuhitaji mtoto wa mbwa.”
Ilibidi Michael ampe tabasamu rafiki yake wa zamani. Inaonekana kuwa mapenzi ya Kane kwa wanyama hao haija fifia kwa miongo hiyo yote.