Sura ya 1-1

2018
Sura ya 1Miaka 10 baadaye… Muziki wenye kelele ulipiga kwa mdundo kutoka kwenye kilabu, alama yake kubwa ya neoni ya rangi ya zambarau ikibadilisha rangi kulingana na mdundo. Taa hiyo ilionyesha mwangaza wa kutisha kwenye jengo lililokuwa ng’ambo ya pili ya barabara. Juu ya paa ya jengo hilo, mtu mweney nywele fupi, za rangi ya kahawia alisimama na mguu mmoja ukiegemea pembeni. Aliinama mbele, kiwiko chake kikiwa kwenye goti lake lililokunjwa, wakati akivuta sigara. Kane Tripp aliinamisha kichwa chake na akapitisha mkono kwenye nywele zake fupi. Alichukia kuzikata, alitamani vile zilivyokuwa ndefu. Bado alikumbuka jinsi zilivyokuwa kama hariri zikiteremka hadi kwenye kiuno chake. Akiinua sigara midomoni mwake, akaivuta kwa undani akijua kuwa alikosa vitu vingi, kama vile sigara alizokuwa akivuta kabla ya kuzikwa hai na akaachwa kufa. Miaka arobaini iliyopita alipatikana bila kutarajia na Malaki, kiongozi wa ukoo mdogo wa chui, na akatuhumiwa kumuua mwenzi wa mbadili viungo huyo. Kabla ya usiku huo, Kane alikuwa na msimamo mzuri kati ya chui, na kiongozi wao alikuwa mmoja wa rafiki zake wa karibu. Midomo ya Kane ilikuwa miembamba kwa wazo hilo. Malaki alimshtaki na kumhukumu, kwa hasira kali. Akitumia fingo kutoka kwenye kitabu ambacho Kane alifikiri alikificha vizuri, Malaki alimfunga na laana, asiweze kusongea au kuongea… asiweze hata kujitetea. Kisha alikiondoa kipuli cha jiwe la damu cha Kane kilichompa uhuru wa kutembea mchana. Hayo mawe ya damu yalikuwa yakimilikiwa na mfyonza damu wa kwanza, Syn. Kane aliuliza wakati mmoja kuwa ilikuwaje kulikuwa na wa kwanza na jibu lilishangaza. Syn alikuja kwenye ulimwengu huu peke yake, akiwa amejeruhiwa na akiwa na njaa. Kijana mmoja alimpata na katika hali yake ya njaa, Syn alichukua damu yake. Mfyonza damu alijifunza kwa haraka kuwa wanadamu wa ulimwengu huu walikuwa viumbe hafifu, ambao nafsi zao zingewatoka ikiwa angeshiriki damu yake, kwa matarajio ya kuunda familia kwenye sayari hii. Lakini mara tu nafsi zao zinapoondoka, walikuwa hawafai tena kwake na huwa karibu na majitu. Wakati wa maisha yake yasiyo na mwisho, Syn alipata wanadamu watatu tu aina hiyo ambao nafsi zao zilisalia… wakawa watoto wake. Tofauti ya pekee ilikuwa ni kwamba, baada ya kugeuzwa, jua linge wachoma… kuwaacha na ndugu za majitu kujificha kutoka kwa jua la mchana. Hili halijakuwa tatizo kwa ulimwengu wa Syn kwa sababu ya jiwe la damu. Vitambaa vinene vya mkono alivyokuwa amevaa Syn vilitoka kwenye ulimwengu wake na vilikuwa vimetengezwa na jiwe la damu. Akirarua kipande cha moja wapo ya vitambaa vya mkono, akakiunda kuwa pete, mkufu, na kipuli kimoja. Kane kwa mara nyengine aliinua mkono na kugusa kipuli alichokuwa amekivaa. Wakati jiwe la damu limempa maisha yasiyo ya kawaida… kilikuwa kitabu cha fingo cha Syn ndicho kilichokuwa kuanguka kwake. Syn alimwachia mchaguliwa wake akitumie kibusara wakati alipolala. Ndani yake kulikuwa na fingo ya uharibifu, njia ya kuwaangamiza watoto wasio na nafsi ikiwa watakuwa hatari kubwa kwa wanadamu. Wakati fingo ya uharibifu ilipotumika kwake, Kane aliweza tu kutazama na macho meusi, yasiyo pepesuka wakati rafiki yake wa zamani akimfunika na mchanga mweusi. Kitu cha mwisho alicho kumbuka kukiona ni anga ilio jaa nyota juu ya msitu wa miti. Giza lilikuwa la kumeza na kimya mno. Fingo lilimfunga lakini aliweza kuhisi vitu kwenye ardhi vikimtembelea. Viumbe hai, vidogo vilivyohepa kula nyama yake isiyokufa lakini bila kujua walitafuna nafsi yake. Muda ulipopita, alifikiri kwa hakika ameshikwa na wazimu, kisha akaanza kusikia sauti mara kwa mara… sauti. Alizikaribisha kwenye gereza lake na akatamani kusikia zaidi. Wakati mwengine alisikia familia nzima, na wakati mwengine alisikia watu wazima peke yake. Wakati mwengine alijaribu kupigana na fingo, kuitisha msaada au hata mtu mwengine awe naye. Uchawi ulimshika kabisa, ukamfanya awe bila nguvu zozote. Alijua fingo hii… aliitumia kwa majitu. Ilikuwa aina ya uchawi tata ambao ulihitaji damu ya mpendwa kumuachilia. Fingo ya mapenzi yenye nguvu ambayo inaweza kuvunjwa tu na mwenzi wa roho wa muathiriwa. Imekuwa ikifanya kazi kila wakati na wafyonza damu wasio na nafsi kwa sababu lazima uwe na nafsi ndipo uweze kumuita mwenzi wa roho. Alikuwa ametumia fingo hiyo zaidi ya mara moja kuwatoa duniani ndugu zake wauaji wasiokuwa na nafsi wasiojua chochote isipokuwa tamaa ya damu. Kane alicheka kwa jeuri akikumbuka wazo la kutisha akijua ameangamia… kwa sababu hakuwa na mwenzi wa roho. Angalau, hakuwa amekutana na fumbo kama hilo. Na ikiwa alikuwa na mmoja, basi ilikuwa haiwezekani kuwa angepita tu juu ya kaburi lake wakati alikuwa akitokwa na damu. Malaki alivunjika moyo sana… alimpenda mke wake sana na alimtaka Kane ajue kina cha mapenzi kama hayo na ayatamani. Na kweli aliyatamani. Mara nyingi angetoa machozi, akimuomba mungu yeyote ambaye angesikia, kumletea mwenzi wake wa roho ili aweze kuwa huru. Kama angekuwa amemuua mke wa rafiki yake, basi ingekuwa adhabu inayofaa. Lakini alikuwa hana hatia ya uhalifu kama huo. Usiku mmoja, baada ya kupoteza matumaini yote… aliisikia. Sauti ya kipekee ya mngurumo wa Malaki ilipenya kwenye mazungumzo yake ya ndani kwa ndani, ikifuatiwa na kelele zengine za kinyama za hasira. Kisha kwa mshangao wake, alisikia sauti ya msichana mdogo moja kwa moja juu yake akipiga kelele wasimuumize mtoto wa mbwa wake. Mlio wa sauti yake ndogo, iliyokuwa na uoga ilivunja kitu ndani yake, ikamfanya atamani kuwa huru, ili aweze kumlinda kutokana na mnyama wa usiku. ‘Malaki hatamuumiza mtoto wa mbwa wako,’ Kane akanong’ona kimoyomoyo. Ilikuwa kweli. Malaki hangemuumiza yeyote isipokuwa walimkosea vibaya sana kwa njia Fulani… hasa mtoto. Akimjua rafiki yake alikuwa mahali juu yake, Kane alihisi cheche ya uhai ikimrudia. Alipatwa na hasira wakati yule msichana alipo piga kelele tena na akasikia kitu kikianguka kwa nguvu kwenye ardhi. Damu… aliinusa damu mbichi ikiingia kwenye mchanga laini kumwelekea. Kilikuwa kitu alichokitamani sana. Harufu ilivamia akili yake na ikamtia wazimu zaidi, akijua asingeweza kuifikia. Alikuwa dhaifu sana baada ya kukuaa muda mwingi bila kinywaji hata kimoja… akisikia kiu hadi kifo na kisha kuto kufa. Hapo ndipo aliposikia kidole chake kimoja kikitingisika. Kane aliweka umakini wake kwenye hili na akaweka nia yake katika kujaribu kusongea. Alisikia siku zikipita, kulingana na jinsi alivyohisi joto juu ya ardhi iliyomfunika. Harufu ya damu ilimzunguka sasa, ikimuendesha mbele. Hatimaye, aliweza kuichezesha mikono yake na kwa pole pole akauanza mchakato wa kujaribu kujifukua kutoka kwenye kaburi lake. Siku zaidi zikapita na wakati mkono wake ulipopenya kwenye mchanga, alilia machozi ya furaha. Akijivuta kutoka kwenye mchanga, Kane aliyafungua macho yake na akaangalia juu, akicheka kama kichaa wakati alipoona anga nyeusi na nyota juu yake. Akiangalia chini kwenye mchanga, aliona kipande cha nguo kilichokua na matone ya damu yaliyokauka. Akikiinua, nakukishika kwenye pua yake akivuta harufu ya damu iliyomueka huru. Akiweka ukumbusho wa mwokozi kwa nguvu mkononi mwake, aliunua mwili wake kutoka kwenye ardhi. Malaki na mgeuza viungo ambaye alimuua mkw wa chui walilala wafu hatua chache kutoka kwenye kaburi lake. Akiangalia kuwapita kuelekea msituni, alijua kuwa msichana alikuwa tayari alikuwa ameenda kitambo lakini Kane alishawishika kuwa msichana yule alikuwa mwenzi wake wa roho. Nani mwengine angeweza kuvunja fingo aliyowekewa na Malaki? Akiwamdhaifu sana kumtafuta msichana, Kane alitambaa hadi alipokuwa Malaki, akionekana kumgusa shavuni kwa upole. Akiugeuza uso wake kumtazama, pumzi za Kane zilimtoka kwa kuchanganyikiwa. Malaki alikuwa amevaa kipuli cha jiwe la damu. Kipuli chake! Papo hapo kwa hasira na mwendo wa kasi sana, Kane alisimama nakipuli amekishikilia mkononi. Akimuangalia Nathaniel, mwanamume aliyemwekea mtego, Kane alikusanya giza lililomzunguka kama joho na kupotea kwenye giza. Kane alivuta pumzi na kutazama moshi ukiolea kwenye hewa, ukijikunja mbele yake kabla ya kupulizwa na upepo. Alikuwa amechukua miaka kumi iliyopita akizurura kutoka nchi hadi nchi, bara hadi bara, akijifunza kila kitu alichokikosa wakati wa miaka thelathini ya hukumu yake ya kifungo. Alliijenga nguvu yake tena pole pole, akianza na mtoto wa mbwa mweupe aliyempata akijikunyata ndani ya shimo la mti pale msituni. Alikuwa kipenzi cha mtu na alihuzunika kufanya kitendo kama hicho, lakini hitaji lake la kula lilikuwa zaidi ya hatia yake wakati ule. Ni baada tu ya kula ndipo alitpotambua kuwa yule mtoto wa mbwa alikuwa wa yule mtoto aliye muweka huru. Akihisi cheche kidogo ya uhai ikiwa ingali ndani ya mnyama huyu wa manyoya, alifanya kitendo cha ajabu sana. Alijiuma kwenye kifundo cha mkono, Kane alilazimisha matone machache kwenye ulimi wake wa rangi ya waridi kisha akamlaza mtoto wa mbwa hapo chini akishangazwa na aliyokuwa akiyafanya. Hii haitafanya kazi… ama itafanya? Msichana huyo alimuokoa mara mbili na hata hakujua. Kumbukumbu ya sauti yake ya uoga bado ilikuwa na nguvu ya kumshtua kutoka kwenye usingizi mzito. Alitamani angemuona… hata kidogo tu kuwe na sura inayoenda na sauti inayomsumbua. Akiufikia mfuko wake, aliuchukua mshipi mdogo na akaiangalia alama iliyoumbwa kama mfupa iliyokuwa juu yake. Alilijua jina la familia lakini anwani iliyokuwa nayo haikuwapo tena… imekuwa haipo kwa miaka. Wakati alipojifunza kutumia tarakalishi, alifanya utafutaji lakini wazazi wa msichana huyo walikuwa wamefariki na nyumba ikauzwa. Binti yao, ambaye alikuwa na hakika ndiye aliye muweka huru, alipotea bila kujulikana alipo. Kane alliitupa sigara yake kando ya mguu wake wa kushoto na kuikanyaga hadi kuzima. Aliprudi Los Angeles, alirudi mara moja kwenye kilabu ambacho Malaki alikiendesha na kuishi humo, na kuipata imeuzwa na watoto wake kuhamia kwenye anwani nyengine. Pahali papya hapakuwa chochote ila ghala lililotengwa, lakini chui walilikarabati hivi karibuni na kuligeuza kuwa kilabu cha usiku kulingana na nyakati. Watoto wa Malaki sasa walikiendesha kilabu hicho. Alitikisa kichwa chake akishangaa jinsi Malaki angeweza kumuoa mke mwengine wakati akijua jinsi alivyompenda mke wake wa kwanza. Alikuwa mwenzi wake wa roho na hata kama wabadilisha viungo walijulikana kwa kupenda ngono, mara tu walipokutana na wenzi wao wa roho ilikuwa haiwezekani kumpenda mwengine. Wakati Kane alipoichunguza, alitambua kuwa mke mpya wa Malaki alimzalia watoto wanne kisha akafariki wakati alikuwa akijifungua mtoto wao wa mwisho Nick. Malaki alifariki usiku aliosikia mlio mkuu kutoka ardhini, lakin Kane bado alishisi hamu ya kisasi ikimla kwa ndani. Karibu wafyonza damu wote huzaliwa kutoka kwenye giza nap engine Syn alikuwa amekosea kumhusu yeye kuwa tofauti na ndugu zake waovu. Pengine kupoteza akili yake kwa miaka thelathini ya mateso yalikuwa yamemharibu kiasi ya kuwa sasa hakuwa tofauti. Akili yake ilikuwa bado iko mahali pa giza ambapo Malaki alimweka. Kadri ya Kane alivyo jua, ilikuwa chui ndio waliotoa damu ya kwanza. Sasa alikuwa amerudi kutoa heshima zake vile vile… dhidi ya kabila lote la wabadilisha viungo, kuanzia na watoto wa Malaki. Lakini hatawachia hapo. Baada ya hapo, itakuwa watoto wa mbadilisha viungo aliyemtega… Nathaniel Wilder. Kuunda wafuasi wakumpatia damu haikuwa ngumu. Kane bado alishangazwa na harakati za kichinichini za Wagothi kwenye mtaa wa mabanda. Wengi wao walikuwa wanatamani kuwa alicho kuwa yeye… mfyonza damu halisi badala ya Mgothi aliyetamani kuwa mfyonza damu. Kile alichohitaji tu kufanya ni kumgeuza mmoja wao, kisha kumuacha mjakazi wake asiekuwa na nafsi kufanya atakavyo. Alimchagua aliyekuwa hatari sana kwenye kikundi… yule ambaye alionekana tayari ameishaipoteza nafsi yake kwa giza. Raven, mhalifu, mwanadamu aliyekuwa karibu kuwa kichaa… Mgothi aliyetengwa, ambaye alikuwa na njaa ya damu kabla ya hata kuwa na haja nayo kiukweli. Raven ndiye alikuwa mtu wa pekee aliyemwambia kuhusu wageuza viungo walio wasaliti walivyomsingizia kisha kumzika angali hai. Kane alimueka huru jambazi huyu mjini. Raven alikuwa amekasirikia ulemwengu kabla ya kuzaliwa tena kama mtoto wa usiku na sasa Kane alimpatia njia ya kutoa hasira hiyo. Raven alijichukulia mwenyewe kulipiza kisasi kwa jina la Kane na mfyonza damu asiyekuwa na safsi alitumia uwezo wake mpya kwa kadiri iwezakanavyo. Hakujaribu kumzuia Raven kwa sababu iliingiana kamili na mipango yake ya kuitega familia ya Malaki kwa muanguko. Kwa nini awalinde wageuza viungo kutokana na Raven? Zaidi alichotoa ni kumwambia ijana kuwa hakuhitaji kuwaua wanadamu ili aweze kula, kuwa haikuwa lazima afanye uharibifu wowote, ikiwa hakutaka. Halikuwa kosa lake kuwa Raven alichagua kuua. Mara ya kwanza Raven alipoua ndio ilikuwa mara ya pekee ambayo Kane aliingilia kati, akimshika Kijana huyo kabla ya kumwacha maiti akiwa amelala na alama ya mfyonza damu ikiwa inaweza kuonekana kwa urahisi na wanadamu. Kuwaweka aina yake siri ilikuwa hali ya kujihifadhi iliyokita mizizi ndani yake na alisahau kushiriki siri hiyo na Raven. Kisha Kane akamuonyesha jinsi ya kupasua kwenye alama ya meno ya nyoka na kuifanya kuonekana kama mauaji ya kikatili. Raven alikuwa akiwaweka waathiriwa wake karibu na Densi ya Mwezi ili wapatikane na maafisa wa mamlaka. Ulikuwa mpango mzuri sana. Wafyonza damu wengu walikuwa na asili ya uovu kwa hiyo Kane alitumia muda wake mwingi akiwa hai kati ya wauaji. Kumuona mvulana huyu akiua ilionekana kama kawaida.
신규 회원 꿀혜택 드림
스캔하여 APP 다운로드하기
Facebookexpand_more
  • author-avatar
    작가
  • chap_list목록
  • like선호작