SEHEMU YA KWANZA.

2441 Words
Alionekana msichana mmoja ndani ya Stendi kuu ya mabasi Dodoma akiwa anakokota begi lake baada ya kushuka katika gari lililokuwa linatoka Mbeya kuelekea Dodoma, alihema na kuangaza macho pembeni, aliangalia huku na kule kisha akaona geti la kutokea kuelekea sehemu ambayo alikuwa amedhamiria kwenda. Alikuwa amevalia shati lake la mikono mirefu rangi nyeusi na sketi ya kushona ya kitenge ndefu hadi kwenye vidole vya miguu yake mithiri ya sarawili, kichwani amechana nywele zake kama msichana wa kisabato, alikuwa amechoshwa na mwendo na alionekana sehemu ile ilikuwa ngeni kwake. Bodaboda mmoja alimfuata na kumwambia, “Dada mambo ? Naweza kukusaidia, unaelekea wapi ? “Hapana, asante naelekea UDOM Chuo, “Naweza kukupeleka ndio usijali, Kabla hajajibu aligeuka na kuona kundi kubwa la watu ambao kiuhalisia walikuwa wanakuja na ile ile njia ( ali pause) kidogo mara wakafika. “Alisikika dada mmoja akisema tuchukue Bajaji jamani au mnaonaje?! “Tupo wengi sasa hiyo bajaji itawachukua wangapi au kwa mafungu? “Ndio si tupo kumi hapa watano watano! “Samahani jamani ( aliuliza ) mnaenda wapi !? Alimjibu kaka mmoja, “Tunaelekea Chuo,vipi mbona kama na wewe ndo unaenda au ? “Ndio ndo naenda, basi tukodishe bajaji kama dada alivyosema twende, “Sawa ! Bajaji waliitwa wawili na kuongea nao kisha wakaanza safari, shida imekuja begi la yule dada maana lilikuwa ni kubwa kiasi kwamba hata kwenye bajaji halikutosha, “Mbona begi lako kubwa sana dada ?! ( aliuliza mwendesha bajaji mmoja) umebeba nini humu ( huku akicheka) “Hakuna hata kitu kizito kuna nguo zangu tu , Dereva alilipandisha begi juu sehemu ya kubebea mizigo na kulifunga “Sasa hapa itabidi tu ulipie maana sio kwa huo uzito na barabara yetu hii mbovu mashimo sana! “Mmmmh ! Nilipie tena ? Shilingi ngapi? “Utalipia tu elfu moja, “Samahani kaka nifanyie tu mia tano nakuomba palipobaki Mungu atakuongezea, “Eeeh ! Sawa usijali pandeni twende, Walianza safari kuelekea Chuo huku kila mmoja akiwa hamfahamu mwenzake jinsi inavyotakiwa, alisikika kaka mmoja akisema “Jamani kufahamiana sio vibaya tunaenda sehemu moja au mnaonaje? Mimi naitwa Amon , “Yeah sure mzee , hahahahaha mimi naitwa Jimmy , “Mimi naitwa Rose natokea Mbeya, “Mimi naitwa Yasinta natokea Kilimanjaro Mbona nyie hamjasema mnatokea wapi ( aliuliza Rose) “Anhaaa ! Daah Mimi natokea Dar (alisema Jimmy) “Na Mimi natokea Moro. Au tutaje na shule tulizosoma , “Hahahahahahahahaha ! Walicheka wote , Kisha dereva aliwaambia wadogo zangu mimi naitwa Emma faster ni boda boda hapa ila nimemaliza hapo Barchelor in International Relationship hapo chuo mnapoenda, maisha mtaani ni magumu sana someni ila mkijua kuwa Maisha ya mtaani yanawasubiria kwahiyo kuweni wajanja jifunzeni jinsi ya kusave hela, maisha ni magumu sana mtajua mkishamaliza. “Mmh! Bro umemaliza hapa UDOM ?! (Kwa mshangao) maana na mimi ndo naenda kusoma hiyo course kumbe haina dili eeeh ? Aliuliza Amon “Sio kwamba haina dili hapana , nikisema hivyo nitakuwa nakuvunja moyo lakini naomba uelewe hata mimi kipindi naenda kusoma nilikuwa najua kuna madili mengi sana lakini sio kweli na sio kwamba ajira hakuna zipo ukibahatika utaenda, ila mimi nimekaa mtaani ni mwaka wa tano naenda sita sasa sijawahi pata hiyo ajira, so wewe dogo nenda usome hayo mambo mengine utajua mbeleni maana hata madaktari wapo waliomaliza na hawana kazi hadi sasa hivi na naomba usipange kusoma ili uje kuajiliwa mdogo wangu , soma ili ujiajiri. “Dah aisee ! Hii ni hatari sema freshi kaka ngoja tu tukasome ili tumalize maana elimu yetu nayo sasa hivi imekuwa na changamoto nyingi ajira hakuna tunasoma tu haina namna , “Komaa , yani komaeni wote maisha sio kama mnavyoyaona sasa hivi utayaona badae baada ya kumaliza Chuo na kurudi mtaani hahahahaha, Aisee tumefika ndo pale , niwapeleke kabisa Administration au niwaache? “No tupeke kaka ( alijibu Rose) “Sawa ingawa mlikuwa tayari tu mmefika, Amon, “Naam Bro,! “ Usione elimu haikusaidii chochote sawa eeeh , hii nawaambia wote ,someni ili tu mpate kuheshimika pia kuweni makini maisha ya Chuo kuna changamoto nyingi sana na maisha ya kila aina , Hakikisha una graduate with A and not HIV/AIDS positive, “Okay Shukrani Brother, “Asante Kaka kwa ushauri Mungu akubariki ( alisema Rose) “Amina , haya jamani mwisho ndo hapa tunaweza kushuka, Walishuka mdogo mdogo lakini Yasinta alikuwa kimya sana na Jimmy kipindi yale maneno ya dereva yanaingia akili mwa Rose na Amon, “Dah huyu bro kanitisha, graduate with A and not HIV/AIDS positive nimeambiwa na brother angu kipindi nakuja, (alisema Jimmy akiwageukia Amon na Rose) “Anhaa nyie mnaogopa nini bhna haya maneno nimeyasikia sana ila watu wanakuja wanasoma na kuondoka emu potezeeni bhana ,(alisema Yasinta) “We Yasinta yule mkubwa ni kaka yetu huenda aliyoyasema yana ukweli na kumbuka amesoma hapa sasa wewe ukisema tupotezee haina maana cha msingi ni kumuomba Mungu atuepushe na haya majanga kudumu katika maombi na kuyaishi maisha yanayompendeza Kirsto Yesu,(alisema Rose) “Wote walishangaa! “Mmmh jamani sawa, hahahahahaha ( alicheka Yasinta) “Usicheke Yasinta unahisi ni mazuri haya ? (Aliuliza Jimmy kwa ukali) emu twende bhana , Waliondoka kuelekea utawala kwaajili ya kuripoti na kuendelea na shughuli zingine za usajili, waliingia ofisini kila mmoja akiwa na viambatanisho muhimu ambavyo vinahitajika kama walivyokuwa wameelekezwa kwenye joining instructions, waliendelea na shughuli hiyo na mwisho hawakumaliza ila walikutana na watu wengi first year wenzao na kubadilishana mawazo huku wakiogopana maana hakuna aliekuwa anajua nani ni nani kila mmoja alimuogopa mwenzake. Rose alikuwa amekaa peke yake huku akiwaza maneno ya yule dereva mara akaenda Yasinta na kumuuliza,, “Mbona umekaa alone unawaza nini ? “Hapana Yasinta hata siwazi chochote nipo tu , lakini ujue najaribu kufikiria yale maneno ya yule dereva mmh ( aliguna) “Bhana wewe nae ujue unaumiza sana kichwa kisa yale maneno ? Mfano wewe hujielewi? Una miaka mingapi na kwanini unakaa unawaza mambo ya watu na kama ni hayo mambo wangapi wameambiwa lakini wanasurvive na maisha yanaenda kila siku yani kama utakuwa na tabia za kijinga unaweza kukutana na hizo changamoto lakini kama ni mtu mstaarabu huwezi kutwa na hayo majanga, kwanza ndo kwanza hata siku hatujamaliza ushaanza kuwaza hayo mambo,.emu tuondoke hapa kuna rafiki yangu kanipigia hapa nimesoma nae shule moja, “Sawa Yasinta mimi nipo makini lakini nahofia wengine ambao hawako kama mimi, “ Emu ! Hivi wewe ukisema uanze kumhofia kila mtu si utakuwa mama huruma sasa khaaa watu wanajielewa ujue na hapa ni Chuo kila mtu ana akili yake wengine wameolewa, wana wachumba wengine wanapata hapa wachumba sasa ukae unawawazia watu kama hawa jamani utateseka mama huruma, hahahahahahahaha. “Hahahahahahaha ! Jamani ndo hadi jina ushanipa haya basi usijali, Ghafla simu yake iliita mlio wa Tecno “Hello “Hello mama shikamoo? “Marhaba ! Hujambo mwanangu? “Sijambo mama nashukuru Mungu ni mwema nimefika salama ila ni mbali mmmh, “Tushukuru Mungu kwa kila kitu mwanangu cha muhimu umefika salama , “Ndio mama nashukuru kwa hilo vipi nyumbani wazima, Anitha alikuwa analia alinyamaza hahahahahaha ila huyo mtoto ananipenda na atanimiss sana, “Hahahahaha ! Amelia katoa kila chozi kasoro la damu na amenyamaza kila mara dada , dada ila amenyamaza,basi sawa mwanangu nilitaka kujua kama umefika na kama nilivyokuelekeza uwe makini na mtangulize Mungu kwa kila kitu chako, “Sawa mama nitafanya hivyo wala usijali, wasalimie wote nyumbani, “Sawa mwanangu zimefika uwe na jioni njema, “Sawa mama na wewe pia, Waliagana na kumaliza yale maongezi kisha safari ya kuelekea hosteli ilipamba moto maana ni mbali sana na utawala hivyo iliwabidi tena kupanda daladala ili kufika na walifanya hivyo , njiani Rose anamuuliza Yasinta, “Nyumbani kwenu ulisema ni wapi vile Moshi au Kilimanjaro ? “Kilimanjaro, “Anha natamani nifike huko ntaenda siku moja aisee ndo kuna baridi sana kuliko kwetu kweli? “Hapana baridi ya kawaida , kwenu Mbeya baridi ni ya kutisha, “Hahahahaha hahahahaha (walicheka wote) alafu akina Amon wako wapi alafu hata namba zao hatujachukua jamani kweli tutawapata? (Aliuliza Rose) “Usijali tutaonana tu maana mimi na Amon tupo course moja lazima tuonane, hivi na wewe Rose unasoma course gani? “Mimi nasoma BAED “Anhaaa unaonekana tu , hahahahaha “Kwanini jamani? “Si unaonekana tu jamani sura yako ya upole, huruma na hata mavazi yako, “Sawa bhana ndo hivyo. Hatimae walifika na Yasinta alifanikiwa kuonana na rafiki yake Irene wa kitambo sana ambae walisoma wote shule ya msingi walifurahi kuonana na kukumbatiana, “Woooh jamani Irene,(walikumbatiana) “Woooh ! Yasinta, nimefurahi kukuona, mmmh unazidi kuwa mrembo jamani, “Asante Irene ila wewe ndo kiboko, huu weupe shoga angu mbona hukuwa hivyo au ndo unajichubua ,hahahahaha hahahahaha “Kujichubua hiyo kwiooo, si nilkuwa hivi jamani hukumbuki nilikuwa mweupe mimi darasa zima Hahahahahahaha, “Mmmmh sawa bhana , Milima haikutani ila binadamu tunakutana, Irene “Yeah shoga angu ni muda tangu tumemaliza la saba eeeh nikahamia Mwanza, “Acha tu ila umependeza ( alianza kumuonea wivu Irene) shoga angu huyo bwana uliempata anahudumia vilivyo, “Hahahahaha hahahahaha ( waliangua vicheko wote huku wakipigana mikono) “Una mambo wewe hujaachaga tu mbona hata bwana sina shoga angu, “Mmmmh shoga angu sasa hapa tunadanganyana ulivyo mzuri ( pisi kali ) ukose bwana kweli na ulivyopendeza hivyo nani kahudumia? “Hehehehehehehee, shoga nina Baba na Mama wote wazima wa afya wanahudumia, sitaki stress mimi na mabwana sitaki kabisa napumzika wanaume hawaaminiki, “Eeeeh ! Usiniambie bibi wewe , kulikoni hawaaminiki na lifetime wako uliekuwa unatusumbua eeeh dada wewe watu hatupumui leo yamekuwa haya hawaaminiki? Hehehehehe, “Shoga acha God nilimpenda sana ila kwa alichonifanyia hapana, siwezi kumsamehe wanaume ni wapumbavu sana, “Eeeeh ! Ilikuwaje nini alichokifanya shoga? “Tuachane na hayo nitakwambia siku nyingine ila elewa tu nimeachana nae nina miezi miwili sasa tangu tuachane, “Heheheh , ama kweli Dunia simama nishuke, yani wewe umeachana na God !? Basi kila mtu ataachana na mtu wake na hakuna mahusiano yatakayodumu. “Ndo hivyo shoga angu , sikuwa na jinsi zaidi ya kuachana nae, Haya sawa huyu hapa anaitwa Rose ni rafiki yangu, Rose huyu anaitwa Irene ni rafiki yangu sana nimesoma nae darasa la kwanza hadi la saba , then akahamia mwanza ndo tumekutana hapa leo tangu tumehitimu darasa la saba, “Oooh wow ! Mungu mkubwa sana , nafurahi kukufahamu Irene, “Asante na mimi pia, Kisha walitembea kuelekea chumbani kwao. ******************************************** Huku Amon na Jimmy nao waliongozana na wenzao kutafuta sehemu ya kulala yani hostel. Walifika hostel lakini wakiwa na maswali mengi sana kichwani wanajiuliza wenyewe , Amon alikuwa ni mstaarabu na hapendi starehe na outings za usiku tofauti na rafiki yake Jimmy ambae anapenda sana outings za usiku na wasichana na ujanja ujanja mwingi kama inavyojulikana watu wanaotoka Dar huwa wanahisi kuwa wanafahamu kila kitu katika hii Dunia kwahiyo Jimmy alikuwa ni kijana mwenye mambo mengi ambayo kama Amon angejua sidhani hata kama angekuwa karibu nae lakini kwa kuwa ndo wamekutana kwanza hivyo hawezi mtambua kwa lolote. Wakati wanatembea Jimmy alikutana na rafiki yake waliosoma nae Advance Tandahimba Sec na kusalimiana kwa hapa na pale lakini ni watu ambao walikuwa hawewezi kukaa katika zizi moja , rafiki yake anaitwa Martin yeye anapenda sana mambo ya Mungu pia ni mstaarabu ila ana mambo yake chini chini kwahiyo mara nyingi hutumia muda wake katika muziki na anapenda kupiga kinanda na Ngoma za kanisani wakati wa nyimbo za kusifu, walisalimiana kisha aliondoka na kuwaacha Jimmy na Amon. Martin aliongozana na rafiki zake wawili Steve na Clement wakielekea kula cafteria kisha walirudi kulala na hiyo siku watu walitembea kwa makundi makundi sana wale waliokuwa wamesoma shule moja advance walirudi hostel kulala na walilala katika chumba kimoja Block “S”, wakiwa wamelala Martin alianza kuwaambia stori za rafiki yake Jimmy.. “Oyah yule jamaa muoneni tu hivyo kwanza anapenda pombe, sigara , wanawake na anapenda kinouma kwenda clubs usiku kipindi tupo advance lazima kila ijumaa atoroke aende kwenye vigodoro vya wamakonde,hahahaha ni nouma kaka na yule mshikaji wake nahisi atakuwa hamfahamu, “Duh ! Kumbe mmeschool nae mshikaji? “Ndio kaka , Daah may be awe amechange saivi, maana mimi zilikuwa haziivi kiivyo mzee sema basi tu katokea Dar alafu ni family friend siwezi kumkaushia alafu si unajua sisi wanaume, “Yeah kweli mzee ila atakuwa amebadilika may be ( aliongea Steve huku stori nzima nae kama inamgusa maana ana sifa kama za Jimmy) maana kuacha pombe na wanawake ni kazi sana kaka ? “Ila mimi sioni hata maana ya pombe ujue zaidi tu ya kudharirishana na kumaliza pesa , sasa mfano unapata boom lako laki 5 mzee ukienda kutumia kwenye pombe itabaki shilingi ngapi si itakuwa haitoshi kabisa mzee , tuweni makini pombe na wanawake ndo kitu kinachosababisha vijana wengi hatufanikiwi ukipata tu pesa unawaza tu pombe na mademu mara kwenda club kitu ambacho hakisaidii yani starehe ya siku moja ni bora hata hivyo hela ungeinvest sehemu flani ili kiwe hata kinakulipa hata elfu 10 kwa wiki sio mbaya kuliko pombe na mademu,( aliongea Martin kwa uchungu sana na kusisitiza), “Dah kweli kaka unachokiongea tunapotea sana kisa pombe ila ndo huwezi kumshauri mtu aache pombe ni vigumu hahahahahahah, “Sikia Martin kama hujawahi kunywa pombe naomba usije ukajaribu kabisa maana ni kama shetani nakwambia, “Hahahahaha ! Kwanini mzee ? “Ndo nimekwambia usijaribu kabisa wewe piga tu kinanda na Ngoma kanisani inatosha, yani kuacha pombe kwa watu wengine ugumu wake ni kama utakavyoombiwa uache kupiga kinanda na Ngoma au usiende church! Hahahaha je utaweza? “Hahahahaha , dah kiukweli siwezi kaka nakwambia tu ukweli’ “Basi ndo kama ilivyo pombe kuacha ( alikuwa anaongea Steve huku Clement akiwa zake kimya anawasikiliza), “Ila pombe ni mbaya jamani acheni ila kibaya zaidi ni kubet, hahahahahahahaha “Hahahahahahaha ( walicheka wote ) Usiku ulikuwa mrefu sana kwao maana walipiga stori nyingi ambazo kiukweli kuisha ilikuwa ni ngumu na walianza kusinzia mmoja kila walilala. Upande wa pili kwenye chemba ya Jimmy na Amon walikuwa wana maongezi nao Jimmy anauliza, “Kaka unayaonaje mazingira ya huku ? “Pako vizuri kaka naona hata hostel zao nzuri sio kama advance, “Ivi ulikumbuka kuchukua namba ya Yasinta na Rose kaka ? “Hapana kaka ,wale wapo tu tutaonana hata kesho kwenye registration hata usiwe na wasiwasi, “Okay ila Rose wa moto mzee yani kama sio ule usukuma na unyasa wake basi tu ? “Anhaaa ! Kaka ushaanza kumtamani Mama paroko si unaona kabisa yule ni Mama mchungaji mtawezana kweli au unataka ufanye njia tu, “ Yule ni mzuri sema tu matunzo , alafu maisha yanatofautiana ujue na huenda kapigwa ushauri wa kutosha mzee , kwamba huoni ilivyo pisi kali kaka ? “Naona ila hamtawezana yule kwanza yupo sensitive na maisha ya chuo yule hataki matani ashapewa ushauri kama millioni ivi,! Waliendelea kupiga stori za hapa na pale mwisho kila mmoja alipitiwa na usingizi. ***************************************** Asubuhi kulipo kucha kila mmoja alijiandaa na kuelekea kwa ofisi za utawala kwaajili ya kumalizia usajili, walikutana tena na Rose na Yasinta wakiwa pamoja na kusalimiana kisha kila mmoja alikaa kusubiri zamu yake ya kuingia ofisini. Hadi majira ya saa 8 mchana Rose na wenzake wote walikuwa wamemaliza usajili na hivyo walikabidhiwa vyumba maalumu ya kulala tofauti na vile vya mwanzo bahati nzuri wote Rose na Yasinta walipata Block “L” ambayo walilala wote ila rafiki yake Yasinta , Irene yeye alipata Block nyingine chumba kingine kinachofuata ila Block ilikuwa ni hiyo hiyo moja. Kama ilivyo kwa akina Jimmy , Amon , Clement,Steve na Martin wote pia walipangwa katika Block moja ila vyumba tofauti kasoro Jimmy na Amon ambao walipangiwa chumba kimoja, maisha yaliendelea na kila mmoja alijihisi kuwa ni mwanachuo, waliitwa kwenye orientations na kutambulishwa maeneo muhimu ya Chuo pia kutambulishwa viongozi na mfumo mzima wa uongozi ulivyokaa na kisha walitawanyika kwaajili ya shughuli nyingine za kila siku kila mtu alifanya usafi hiyo siku lakini ili kujiandaa na kesho yake darasani kila mmoja akiwa na shauku ya kutumia vyumba ya University of Dodoma, walipiga picha mbalimbali wakiwa pamoja na jioni walipata chakula kwa pamoja walibadilishana namba na kisha kila mmoja aliishia katika chumba chake cha kulala.
Free reading for new users
Scan code to download app
Facebookexpand_more
  • author-avatar
    Writer
  • chap_listContents
  • likeADD