Sura ya 2Kat alikuwa amesongea na kusimama kando ya dirisha. Alitaka kuwa mbali sana na Quinn kama awezavyo. Karibu ayazungushe macho yake alipogundua kuwa kusongea kwake kulimleta tu kwenye upeo wa macho yake. Alitamani kuwa Envy angekuwa hapa. Alihitaji kuongea na yule mwanamke mwengine… au mwanamke tu mwengine kwa jumla. Ingekuwa bora katika mazungumzo haya yaliyojaa hoja za wanaume.
Akiangalia kote chumbani, alitambua kuwa sio wakuu wote wa jamii ya simba walikuwepo.
“Micah na Alicia wako wapi?” Kat aliuliza akijua walipaswa kuwa sehemu ya hiki… chochote kilicho kuwa.
Quinn alimuangalia Warren kwa muangalio ambao alidhani kuwa yule chui atauelewa na kumsaidia kwa kile alichokuwa tayari kukisema. “Alicia haja rudi kutoka shule ya bweni tangu mwezi mmoja na hatumleti katika vita hivi. Ni hatari sana kwa wasichana.”
Uso wa Kat uliingia Weusi zaidi na alionekana kuwa tayari kukirarua kichwa cha jamii ya simba.
“Na Micah?” Warren aliuliza kabla Kat kuwa na wakati wa kuanza vita baada ya msemo wake wa mwisho.
“Hapatikani,” Hasira iliyokuwa kwenye sauti ya Quinn ilimfanya kila mmoja amuangalia kwa kutaka kujua. “Tumejaribu mara kadha kumpigia simu lakini anakataa kuishika simu yake.”
Stefano alivuta pumzi kwa ule ujeuri wa Quinn na kumkatiza, “Micah hajapatikana kwa zaidi ya majuma mawili.”
“Nini?” Warren akiwa amekasirika kwa ghafla. “kwa nini hamkutuita kwa msaada?”
“Kwa sababu ya jariba pumbavu,” Kat alikejeli. “Ni wazi kuwa aliogopa kuwa hatungeweza kukabiliana na lililosema kwa sababu ya hali zetu za hasira.”
Michael alikitikisa kichwa akijua kuwa hadi familia hizi mbili zitakapo suluhisha tofauti zao, itabidi awe muamuzi. “Sawa, wakati tunafanyia kazi tatizo la wafyonza damu, pia tuta kuwa macho kutafuta miongozo ya kupotea kwa Micah.”
“Mantiki inadhihirisha kuwa Micah atarudi mwenyewee, huwa anarudi kila mara,” Quinn aliinua mabega.
Kat aliangalia nje ya dirisha akiwa bado amekasiriki. Quinn alithubutu vipi kugusia kuwa wasichana wasihusike? Wanaweza kumweka Alicia kando na haya ikiwa wangetaka, na kweli wanapaswa kufanya hivyo kwa kuwa alikuwa mdogo zaidi kati yao wote. Lakini wakijaribu kumzuia, basi watapata mshtuko mkubwa. Tatizo lilikuwani kwamba, sasa hata yeye alikuwa ana wasiwasi kumhusu Micah.
Quinn angesukuma kila kitu njiani na kuwaita. Alijua kuwa wangemsaidia licha ya tofauti zao. Kwani kuna nini ikiwa baba zao waliuana… dhambi za wazazi hazifai kuwaangukia watoto wao.
Ingawa hakulijua, Warren alikubaliana na Kat kimya kimya. Quinn ange wasiliana nao wakati alipogundua kuwa Micah amepotea. Alikuwa anaijua vizuri jinsi ubishi kati ya ndugu hao huweza kulipuka. Tofauti zao kawaida ziliishia na Micah kutoka nje na kupotea kwa siku nyingi mara moja… lakini sio majuma.
Stefano na Nick waliendelea kuwasiliana kwa miaka hiyo yote na Nick alimjulisha kuhusu yaliyokuwa yakiendelea katika familia ya simba. Wakati Micah na Quinn walipoligana, Micah alimwambia Stefano mahali alipokuwa akienda ikiwa ataenda kwa zaidi ya siku moja. Wakati huu Micah hakuwacha ujumbe na yeyote, kumaanisha kuwa alikuwa haendi kukaa kwa muda mrefu.
“Baada ya kiota hatari cha wafyonza damu mimi na Stefano tulichokipata kanisani, hakuna anayestahili kuenda nje peke yake usiku wa leo. Tunahitaji kuwa wawili wawili,” Quinn alisema akibadilisha mada.
Stefano alijihisi tofauti wakati picha ya yule msichana aliye mpata na kumpoteza usiku ule ilipopita kwenye akili yake. “Nadhani nitarudi kule usiku wa leo na kuhakikisha kuwa lile kanisa bado ni safi. Huenda tukawa tulikosa kuona kitu.”
“Nitaenda na Stefano,” Nick alijitolea akitaka kuwa na muda na rafiki yake wa zamani mkorofi.
Kat aligadhabika kwa muda wakati alipofanya hesabu kimya kimya. Bilas haka, Michael angeenda na Kane, na kwa kweli hangependa kuungana na Kane kwa sababu alikuwa mbali na kuwa kamili. Hiyo ilimuacha Warren na Quinn.
“Nitaenda na Warren,” Kat alijitolea.
“Hapana,” Warren alimrekebisha. “Tunamhitaji mtu kukiangalia kilabu.”
“Ati kwa sababu mimi ni msichana hai maanishi kuwa siwezi kujisimamia,” Kat aliwaonya, kisha kwa utaratibu akatoka nje ya chumba.
Wanaume wote chumbani walijikunja wakati alipofunga mlango taratibu nyuma yake.
“Wue,” Nick alinongóneza. “Natamani hata angeufunga mlango kwa nguvu.”
Steven na Quinn hawakuwa wamemuona Kat kwa miaka michache lakini wangeikumbuka hasira yake vizuri sana. Kuufunga mlango taratibu nyuma ya Kat aliyekasirika ilikuwa mbaya zaidi mara kumi kuliko Kat aliyetoka nje kwa fujo. Alikuwa amekasirikia… la, alikuwa ameipita sehemu ya hasira. Alikuwa amekasirika vibaya.
“Ninaenda kumpigia Devon simu na kumfahamisha kuhusu yanayoendelea,” Warren alisema na kuivuta simu ya mkononi kutoka kwenye mfuko wa suruali yake. Hakupenda kumfanyia ndugu yake hili lakini ikiwa hangefika nyumbani hangukuwa na nyumba ya kurudia. Akiibonyeza nambari kwenye simu, alitembea kuelekea mlango tofauti ulioelekea kwenye chumba cha kulala.
Warren alisubiri wakati simu upande ule mwengine ikiendelea kuita. Mwishowe alimsikia mtu akiishika na kulaana mara tu baadaye.
“Unataka nini?” Devon aliuliza akisikika kuwa na usingizi lakini mwenye furaha.
Warren kwa haraka alimjulisha yaliyofanyika tangu Devon na Envy kuondoka chini ya saa ishirini nan ne zilizopita.
Devon alipumua, “Jamani, nauwacha mji na kila kitu kinaharibika.”
“Nitakupa siku chache kisha unahitaji kuwa nyumbani.” Warren alisema. “Pia ninakuhitaji unifanyie kitu kimoja katika muda huo wa siku chache.”
“Ni nini hilo?” Devon aliuliza akisikika kuwa macho zaidi.
“Ninahitaji umuulize Kriss ikiwa atatusaidia. Mwambie Dean tayari amekubali lakini kwa hakika tutamuhitaji, pia. Ikiwa itabidi, mwambie Envy amshawishi Tabatha kuwa tunamhitaji Kriss hapa kwa sababu ulingana na ninayo yasikia, ikiwa atarudi basi yule aliyeanguka atamfuata.”
“Nitaona nitakalo weza kulifanya,” Devon alisema. “Kriss ni mtu wa ajabu. Unajua, yeye hutembea kwa mdundo wake mwenyewe.”
Warren alitikisa kichwa, “Ananikumbusha mtu mwengine ninaye mjua.”
Devon alicheka, “Sawa kaka, lakini si ahidi chochote.”
“Nitakuona siku chache zijazo.” Warren alisema na kuikata simu.
*****
Quinn alimtambua Kat kwenye viwambo vilivokuwa kwenye ukuta. Kwa kuwa kila mmoja alikuwa akimsubiri Warren amalize kwenye simu yake, alisongea karibu na kiwambo kana kwamba alikuwa amesinywa. Kusinywa siyo hali aliyoihisi wakati alipokuwa akimuangalia Kat.
Alifikiria kuwa alikuwa mrembo miaka kadha iliyopita, lakini alikuwa hakukisia kwa ukamili kile angegeuka kuwa. Miaka iliyoendea alikuwa akimuangalia Kat kwa mbali. Hata alikuwa ameajiri wapelelezi kufanya kazi hapa kwenye Densi ya Mwezi na kumpa ripoti… ingawa yule wa mwisho aliye mtuma aligeuka kuwa mmoja wa waathiriwa wa mauaji.
Alijikunja wakati mtu mmoja alitembea hadi mahali alipokuwa Kat amesimama na kuufikia mkono wake. Kulingana na vile kamera ilifyokuwa imewekwa, Quinn alihisi kuwa yule mtu hakuwa katika hali ya urafiki.
*****
Trevor aliingia ndani ya kilabu cha Densi ya Mwezi asijue ikiwa alitaka kukiharibu kilabu hiki au kuizika hasira yake kwenye galoni kadha za pombe. Alijaribu kuwasiliana na Envy lakini ilikuwa Dhahiri kuwa alikuwa anajificha. Tabatha na Kriss pia inaonekana kuwa walikuwa pia wakizihepa simu zao pamoja nay eye. Alipomuuliza kaka yake aliyejua yote mahali Envy alipokuwa, alitamani kukirarua kichwa cha Chad wakati hakuwa wazi kuhusa mahali alipokuwa.
Trevor alimuona Kat akitoa vinywaji nyuma ya baa ile ile aliyofanya kazi kwa kawaida. Alimfikia na kuushika mkono wake ilikuupata umakini wake lakini jinsi alivyomuangalia kulimfanya arudi nyuma na kukaa chini.
“Ile ya maalum kwa vipiga shoti imeisha. Je, ninaweza kukupatia kitu chengine? Kama uanachama wa maisha katika moja ya baa zile zengine?” Kat alipepesa nyusi zake bila hatia. Mwishowe akimuangalia machoni na kuuona unyonge ukiogelea pale aliinua bega, “Samahani, mlengwa wangu wa kweli yuko mbali. Nikupatie nini?”
Trevor alikisugua kipaji cha uso wake kwa ncha ya vidole vyake. Atashangaa ikiwa angeweza kufumbua fumbo la jinsia hii. Sio kuwa wali yafanya mabo kuwa rahisi. “Majibu fulani yatanisaidia.”
“Kama?” Kat aliuliza.
“Kama mahali alipojificha mpenzi wangu.” Aliinua nyusi kidogo wakati akisubiri.
“Mpenzi wako? Umeisha mbadili Envy haraka hivyo?” Kat alitabasamu wakati alipomkazia macho kimya. “Oh, unamaanisha Envy.”
“Unadhani?” Trevor alimjibu kwa mzaha.
“Ni lilolisikia mara ya mwisho ni kuwa mpenzi wako wa zamani na kaka yangu walienda kwa aina ya fungate”. Kat aliinua bega ilikuwa karibu na kweli Envy angefikiria hivyo.
“Ninadhani alikuwa na Tabatha na Kriss?” Trevor alihisi msukmo wa damu ukipanda kwa hali ya hatari akiwaza ikiwa Chad alimdanganya kuhusu hilo.
Kat kwa haraka alimmiminia bilauri moja la Joto akitumai kuwa litatuliza hasira aliyoiona iki waka ndani ya macho yake. “Yuko nao. Tabby na Kriss wako nao.” Alikisukuma kinywaji mbele yake na kuongezea, “Hiyo imesimamiwa na mwenyeji.”
Akimuangalia wakati alipokuwa akikiteremsha kile kinywaji, midomo yake alibaki wazi wakati alipouona mwangaza uliokuwa juu yao ukimulika machozi ambayo hayakuwa yame mwagika yakijaribu kukusanyika ndani ya macho yake.
Hiyo inauma. Mara moja alijuta kumfanyia kejeli. Alitamani Quinn angehisi hivyo kumhisi. Ingekuwa vizuri ikiwa angeonyesha hisia kidogo juu yake au kile alicho hisi kumhusu. Hata angeweza kuisha na Quinn kumpuuza, ikiwa tu angekuwa na ujasiri wa kumwambia usoni mwake.
Akimfikia, aliuweka mkono taratibu kwenye bega la Trevor kisha akafikiria njia ya kuyatoa yale akilini mwake na na pia kumpata mwenzake wa kuwinda naye mara hiyo hiyo.
Kat alitabasamu wakati wazo lilipomjia kichwani. Alimuita chui usiku ule mwengine, kwa hiyo hakuwa akidanyanga kuwa alikuwa mtafiti wa mambo yasiyo ya kawaida. Ikiwa wale vijana walilitaka jeshi, basi aliloweza kufanya ni kusaidia kuandikisha watu… sawa?
“Sasa, ikiwa uta ni ruhusu, ninaenda kujifanya chambo kizuri kwa wale wafyonza damu ambao wamekuwa wakiwacha miili mlangoni mwetu.” Akaanza kutembea kutoka kwenye nyuma ya baa lakini Trevor aliushika mkono wake kwa haraka hata hakumuona akisonga. Aliinua tu nyusi kuuangalia mkono uliyomzuia. “Itabidi uuwache mkono wangu, pengine uje kunisaidia.”
“Una maanisha?” Trevor aliuliza.
Hata yeye pia alikuwa na wazo lile lile kuwa walikuwa ni wafyonza damu kwa sababu kulikuwa na mchipuko wao kwa sasa… oh, na ukweli mdogo wa zile alama za meno zilizoharibiwa nusu. Tatizo la hili ni kuwa alikuwa haja kbiliana na wafyonza damu hapo awali… ni wakati wa mafunzo. Alihitaji sababu ya kukaa pale hadi wakati Envy atakaporudi, kwa hiyo ni kwa nini asikae hapo na mdogo wa mpinzani wake?
Wakati Kat alipotikisa kichwa na kuutoa mkono wake pole pole, Trevor alikitikisa kichwa chake akijua kuwa atajutia hili, “Je, kaka zako wanaenda na wewe?”
“Oh, wanaenda kweli, lakini pande tofauti.” Aliukunja uso wake. “Inaonekana kuwa hakuna aliyetaka kujiunga na msichana.”
Kana kwamba kuthibitisha hoja yake, Stefano na Nick walichagua muda ule kuteremka chini na kuelekea mlangoni wakiwa pamoja. Nick alimkazia Kat macho, akitumai kuwa atapata ujumbe na kufanya Warren alichomwambia afanye… kaa hapa ambapo ni salama. Alijihisi nafuu kidogo wakati Kat alipompa tabasamu dogo kana kwamba yote yalikuwa yamesamehewa.
Akiangalia nyuma kwenye mlango ulioongoza kuelekea ghorofa ya juu Kat alitikisa kichwa, “Ona, ni makundi usiku wa leo isipokuwa ile nambari isiyo ya kawaida… kwa jina lengine mimi.” Alimpa Trevor tabasamu kubwa kana kwamba hakujali. “Lakini hilo ni sawa, sijali kuwinda peke yangu.”
Trevor alitabasamu na kuikunja mikono yake juu ya baa. Aliinama mbele kidogo akimpa ishara Kat kufanya hivyo hivyo na kunong’oneza maneno mawili.
“Sio peke yako,” alikitikisa kichwa chake.
Quinn na Warren walisimama walipofika chini kwenye kilabu. Warren alijua kuwa walikuwa na wahudumu wengi kupita kiasi usiku wa leo kwa hiyo baa inge simamiwa vizuri lakini hilo halikumzuia kutoa maagizo machache mara ya mwisho.
Wakati alipokuwa akifanya hilo, Quinn karibu atoboe shimo kwenye mgongo wa Trevor kwa macho yake. Hakukikosa kiwambo, kuona jinsi Trevor alivyoushika mkono wa Kat… au densi ya kihisia iliyo fuata. Kat alikuwa na uhusiano wa aina gani na mtu huyu? Jinsi walivyokuwa wakifanya, ilikuwa ni kama walikuwa na siri walio ishiriki ambayo wengine hawaku ruhusiwa kusikia na ilimuumiza mishipa.
“Yule mtu aliye na Kat ni nani?” Quinn aliuliza wakati Warren alipomaliza na kifaa chake cha mawasiliano.
Warren aligeuka na kumuangalia mpenzi wa zamani wa Envy. Aliwaza kuwa Kat alikuwa akimwambia Trevor kuwa Envy alikuwa hapatikani tena, ambalo lilikuwa wazo zuri kwa sababu ikiwa mpenzi wake hatakuwapo kwenye baa, pengine yule mpelelezi wa mambo yasiyo ya kawaida ataenda kufanya uchunguzi wake mahali pengine.
“Huyo ni mchochezi tu anayependa kupigwa shoti na wanawake warembo,” Warren alitabasamu kwa mzaha wake mwenyewe. Kule kuto kutabasamu kwa Quinn kulimfanya akose kule kujiunga na Michael. Aliwaza ikiwa alikuwa amechelewa sana kumbadilisha mwenzake kisha akalifuta wazo lile. Quinn na Kane wakiungana litakuwa janga linalo subiri kutokea.