kijiji chenye laana ,kilicho mpata binti mmojaUpdated at Apr 10, 2025, 23:53
NYUMBA YENYE LAANSURA YA KWANZA: SAFARI YA GIZAUsiku ulikuwa umetanda giza nene huku mawingu mazito yakifunika mwezi. Marietha alishuka kutoka kwenye basi dogo lililomsafirisha kutoka mji wa Makuyu hadi kijiji cha Kagongo. Alikuwa na begi lake dogo mgongoni na mfuko wa plastiki wenye chakula kidogo. Alisimama kwa muda mfupi akitazama njia nyembamba iliyokuwa ikielekea kwenye nyumba aliyokodisha.“Msichana mdogo, hakikisha unakuwa makini na nyumba hiyo,” alisema mzee mmoja aliyekuwa akipita karibu na kituo cha mabasi.Marietha aligeuka na kumtazama yule mzee kwa mshangao. “Kwa nini unasema hivyo?” aliuliza.Mzee huyo alitikisa kichwa na kunong’ona kwa sauti ya chini, “Nyumba hiyo ina historia mbaya. Wengi wameondoka na hakuna aliyewahi kuishi humo kwa muda mrefu bila matatizo.”Marietha alitabasamu kwa upole. “Siogopi. Ni nyumba tu,” alijibu, kisha akaendelea na safari yake.Moyo wake ulianza kupiga haraka alipoikaribia nyumba. Ilikuwa ya ghorofa moja, kuta zake zilionekana kuchakaa, na madirisha yalikuwa na vumbi jembamba. Alifungua mlango kwa funguo alizopewa na mwenye nyumba na kuingia ndani. Harufu nzito ya unyevu ilimkumba.Aliwasha taa ya umeme na kuangaza sebuleni. Samani chache zilikuwepo—sofa la zamani, meza ya mbao iliyochakaa, na kabati la vioo lililojaa vumbi. Alipiga hatua kuelekea chumba chake, akihisi kama kuna macho yaliyokuwa yakimwangalia.SURA YA PILI: NYUMA YA KUTAUsiku wa kwanza haukuwa rahisi. Marietha alilala kitandani mwake, lakini usingizi haukumjia haraka. Kulikuwa na sauti za mluzi zikitokea nje, upepo mkali ukivuma na kupeperusha mapazia yake kwa nguvu. Mara ghafla, alisikia mlango wake ukifunguka taratibu kwa mlio wa kutisha.Alisimama kwa haraka na kuwasha taa, lakini hakukuwa na mtu yeyote.“Mwenye nyumba aliniambia kuwa hii nyumba ni salama,” alijisemea kimoyomoyo, akijaribu kuondoa woga uliokuwa ukizidi kupanda ndani yake.Lakini kadri usiku ulivyozidi kusonga mbele, sauti za kuhema zilianza kusikika kutoka ukutani. Ilisikika kama mtu aliyekuwa akilia kwa uchungu, kilio cha huzuni na mateso makubwa.Marietha alifunika kichwa chake na shuka, akijaribu kupuuza yale yote aliyokuwa akiyasikia. Lakini mara moja, sauti nzito ilisikika.“Kwa nini uko hapa?”Aliruka kitandani na kuwasha taa. Hakuona mtu yeyote. Mapigo yake ya moyo yalikuwa yanakwenda kwa kasi.Hakujua kuwa usiku huo ulikuwa mwanzo tu wa mateso yake…---SURA YA TATU: HISTORIA YA NYUMBAMuda mfupi baada ya kuhamia, Marietha aliamua kufanya utafiti kuhusu historia ya nyumba ile. Alienda kwa mzee mmoja kijijini aitwaye Babu Chalo, ambaye alionekana kuwa na maarifa ya kale kuhusu nyumba hiyo.“Kabla hujazaliwa, nyumba hiyo ilimilikiwa na familia ya Bw. na Bi. Kasimba,” Babu Chalo alianza kusimulia. “Walikuwa watu wa kawaida, lakini walihusishwa na vitendo vya ushirikina. Kila usiku, jirani zao walishuhudia moshi ukifuka kutoka kwenye vyumba vyao vya chini, na sauti zisizoeleweka zilikuwa zikisikika. Siku moja, watoto wao wawili walipotea ghafla.”Marietha alimtazama Babu Chalo kwa hofu. “Walipotea? Walipatikana?”Babu Chalo alitikisa kichwa. “Hapana. Walitafutwa kwa miezi kadhaa lakini hawakupatikana. Baada ya muda, watu walianza kusikia sauti za kulia usiku, na waliowaona Kasimba walisema walikuwa wakihangaika sana. Usiku mmoja, familia nzima ilitoweka. Ilikuwa kama walimezwa na giza.”Marietha alihisi baridi ikipenya mifupa yake. “Kwa hiyo… unamaanisha kuna kitu kilicho ndani ya nyumba hiyo?”Mzee huyo alimtazama kwa macho makali. “Si kitu, Marietha. Ni roho zilizofungwa. Na ukikaa humo muda mrefu, utakuwa sehemu yao.”Marietha alishusha pumzi nzito, akijaribu kujihakikishia kuwa haya yote yalikuwa hadithi tu. Lakini usiku huo, aliporudi nyumbani, alivyoingia tu ndani, mlango ulifunga ghafla nyuma yake kwa kishindo kikubwa…Na hapo ndipo alitambua kuwa hakukuwa na njia ya kurudi nyuma…---SURA YA NNE: MSETA NA ANORDBaada ya siku chache, Marietha alipata wageni—ndugu zake wawili, Mtema na Anord. Walikuwa wamefika kutoka Makuyu baada ya kusikia kuhusu nyumba hiyo na hali ya Marietha.“Marietha, kwa nini uliamua kuhamia hapa peke yako?” Mtema aliuliza, akitazama nyumba kwa macho ya mashaka.“Nahitaji kujitegemea,” Marietha alijibu, lakini macho yake hayakuweza kuficha hofu aliyokuwa nayo.Anord alizunguka sebule, akipapasa kuta kwa mikono yake. “Kuna kitu kisicho cha kawaida hapa,” alisema kwa sauti ya chini. “Najua siwezi kuona, lakini nahisi… nguvu za giza.”Mtema na Anord walikaa usiku huo, wakijaribu kumshawishi Marietha waondoke, lakini alikataa. Hata hivyo, usiku ulipofika, wote walishuhudia tukio la kutisha—mlango wa chumba cha chini ulifunguka polepole, upepo wa baridi kali ukitoka ndani, na sauti ile nzito ikasikika tena:“Hamna pa kukimbilia.”Anord alishtuka na kushika kifua chake. “Tunahitaji kutoka hapa, sasa hivi! lakini wakiwa pado hawajachukua hatua yoyote taa ilizima ghafla ,na taa zilozima na Giza totolo likatanda.......wakabaki wakiwa wamepigwa butwaa........