bc

Langas Hustle: The Boda Money

book_age18+
0
FOLLOW
1K
READ
dark
mafia
drama
kicking
poor to rich
like
intro-logo
Blurb

Brian ni boda wa Langas, Eldoret. Kila asubuhi anaamka na deni ya boda, polisi wa traffic, na mama yake mgonjwa.

Siku moja jioni, abiria mmoja wa suti alimwacha bag kwa pikipiki na akapotea. Ndani ya bag hakukuwa na nguo, ilikuwa na pesa mingi na kitu kingine hatari.

Kuanzia hapo, maisha ya mtaa inabadilika. Marafiki wanakuwa maadui, polisi wanamtafuta, na yule abiria anarudi.

Je, Brian ataokoka na pesa au mtaa itamla?

Hadithi ya ukweli ya maisha ya ghetto, hustle, na uamuzi mgumu.

chap-preview
Free preview
Chapter 1: Deni ya Langas
Jina langu ni Brian. Sina kazi ya ofisi, sina degree. Niko na boda tu ya loan na deni kila siku. Langas, Eldoret. Kila asubuhi na-amka na hesabu tatu. Deni ya boda 300, mama anahitaji dawa 500, na polisi wa traffic pale Annex wananingoja na fine ya 1000. Hiyo ndio maisha yangu. Saa kumi na moja alfajiri leo, nimebeba jamaa mmoja kutoka stage. Amevaa suti safi sana, ameshika bag kubwa ya ngozi. Hakuwa anaongea. Aliniambia tu, "Haraka, town, usisimame mahali." Tumefika Eldoret town karibu na Naivas. Jamaa akashuka haraka. Akasema, "Ngoja hapa, narudi na pesa." Akaacha bag kwa pikipiki yangu na akaingia ndani ya building. Nangoja dakika moja, mbili, tano. Hakurudi. Dakika kumi. Hakuna. Simu ikaanza kuita. Ni boss wa boda. Anasema, "Brian, leo hujalipa. Ukichelewa tena nachukua pikipiki." Niko na stress. Nikaangalia bag. Nikasema labda jamaa ametoroka na ameacha kitu naweza uza nirudi na pesa ya boss. Nimefungua zip ya bag kidogo. Sikupata nguo. Sikupata laptop. Ndani kulikuwa na bunduki mbili ndogo nyeusi, na pesa. Pesa mingi sana. Bundles za thao, zimefungwa na rubber band. Na karatasi moja imeandikwa majina ya watu na namba za simu na pesa mbele yao. Moyo ukaanza kugonga kama engine ya nduthi. Kabla sijafunga bag, gari mbili nyeusi zikasimama mbele yangu. Watu watatu wakatoka, wamevaa suti pia. Mmoja akaniuliza, "Kijana, umemuona mzee alikuwa na bag kama hii hapa?" Nikatetemeka. Nikasema, "Hapana, sijaona." Akangalia pikipiki yangu, akaona bag. Akatabasamu kidogo na akasema, "Sawa. Usiwe na haraka. Tutarudi." Wakaingia kwa gari na wakaenda. Sikujua nifanye nini. Kama nipeleke bag polisi, watanishuku mimi ni mwizi. Kama niibebe nyumbani, wale watu watanifukuza usiku. Nikaamua kitu kimoja. Nimefunga bag vizuri, nimeirudisha kwa carrier ya boda, na nimerudi Langas full speed. Njiani polisi wa traffic akanisimamisha pale Cheplaskei. Aliniambia nipe kitu kidogo. Nilikuwa na hofu ataniangalia bag. Nikampa 200 ya mwisho nilikuwa nayo mfukoni na nikatoroka. Nimefika keja yangu Langas. Ni keja ndogo ya mabati. Mama analala ndani, anakohoa. Nimeficha bag chini ya kitanda haraka. Usiku huu sijalala. Niko na maswali tu. Yule jamaa wa suti ni nani? Pesa ni ya nani? Na wale watu wa gari nyeusi watasema nini wakirudi kesho? Na marafiki zangu wa stage ya boda, nikianza kutumia pesa kidogo tu, watajua. Langas ni ndogo, watu wanaongea sana. Nimeangalia dirishani saa saba usiku. Kuna pikipiki moja imesimama kwa barabara ya mbele. Mtu hajaishuka. Amevaa helmet. Ananiangalia tu. Mchezo umeanza. Na mimi sina pa kukimbilia.

editor-pick
Dreame-Editor's pick

bc

Yüzbaşının Cerrahı

read
1.8M
bc

The Silver Wolf

read
669.8K
bc

The Billionaire’s Intern

read
1.2M
bc

Chosen, just to be Rejected

read
924.8K
bc

Inferno Demon Riders MC: My Five Obsessed Bullies

read
1.2M
bc

Claimed by the Biker Giant

read
2.3M
bc

Unscentable

read
2.3M

Scan code to download app

download_iosApp Store
google icon
Google Play
Facebook